Featured Post Today
print this page
Latest Post

Niweze kujikimu,wateja kumi kwa siku...

Mimi ni mwanamke nimeolewa na nina mtoto mmoja,kabla sijaolewa nilikuwa nafanya biashara ya kujiuza(changudoa) na nilifanya hivi ili kupata pesa ya kujikimu maana maisha yangu yalikuwa magumu baada ya mama na baba kufariki.Niilikuwa na uwezo wa kuhudumia hadi wateja kumi kwa siku,hali ile imeniadhiri sana maana Naombeni ushauri wenu wakubwa wenzangu maana hata raha ya ndoa siioni...
0 comments

Ndoa na afya njia panda ..

Habari zenu mimi ni mschana wa miaka 23 nimeshatembea na wanaume 35 na kati ya hao niliokuwa na mawasiliano nao ni watatu tu na kati ya hao kuna mmoja ndo ananihudumia nikimwambia kitu ananifanyia hila anaishi na mwanamke, na mwanamke wake ni mjamzito na yeye huyo mwanaume anasema anataka anioe je nifanyeje wakati na wale wawili waliobaki nao wanasema wanataka waniowe na juzi nimekwenda kupima afya yangu nimekutwa sina maambukizi yeyote ukimwi....
48 comments

Nimekuta 47 nami ndani? niulize?

Nina mpenzi wangu ambaye nampenda sana,wakati tunaanza mahusiano aliniomba chupi yangu na mimi nikampa.Week iliyopita wakati nafanya usafi chumbani kwake nikaona begi zuri mfunguni mwa kitanda...kufungua nikakuta chupi za kike 47 na ile yangu niliyompa ikiwemo.Hebu niambieni nimuulize au nifanyeje?
41 comments

Anasema simpendiii!

Nimeolewa lakini bado sijabahatika kupata mtoto,jamani mume wangu ana tabia ambayo inanichanganya sana..yeye hupenda kufua nguo zangu za ndani(bra na chupi).nikimkataza huwa anakasirika na anasema simpendi.jamani nifanye nini?
2 comments

Kwake yeye ni kawaida kabisa....

Jamani mimi nimeolewa ila tatizo liko kwa mume wangu mara kwa mara nguo zake za ndani huwa zimechafuka na ninapomuuliza ananiambia kwamba eti hiyo ni kawaida kwa wanaume kuna wakati ute unatoka wenyewe,,mie sikuamini hivyo naomba mnisaidie je ni kweli maana nahisi mume wangu anasex nje na mwanamke mwengine.....
1 comments

Dhahabu kitandani?! Nilishtukaaa sana...

Nimeolewa nina watoto wawili.mimi ni nesi na mume wangu ni mhasibu,kama mnavyojua kazi yangu huwa mda mwingine naigia kazini usiku na kurudi asubuhi.Jana niliingia kazini usiku,mume wangu alibaki nyumbani na watoto.Niliporudi asubuhi nilimkuta mume wangu bado amelala kitu ambacho sio kawaida yake.Nilimuuliza kama anaumwa akasema hapana.Basi kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana na mimi nikijitupa kitandani nikaungana na mume wangu nikalala.Nilipoamka sijamkuta mume wangu kitandani.Wakati natandika kitanda nilikuta cheni ya kiunoni ya dhahabu,nilishitka sana maana mimi sina kawaida ya kuvaa cheni kiunoni.Nimechanganyikiwa mwenzenu hebu nishaurini la kufanya.
54 comments

Mbona kishawishiiiiii!!!!!!!!!!


Tangu nimejifungua nahisi hewa inatoka huku mbele. Hali hii hujitokeza ikiwa sijavaa chupi au nguo, yaani nikiinama na kuinuka nasikia hewa inatoa,Sasa sijui nikiinama hewa ndio inaingia na nikiinuka ndio inatoka, hivi ni kawaida au ndio kwisha habari yangu?"Napia hamu yangu ya kungonoka imepotea kabisa,najiona nampa mwenza wangu wakati mgumu sana naogopa nisije mpakishawishi cha kutoka nje,Naombeni msaada wenu je nifanyeje,je kuna tiba?
2 comments

Hii nayo kubwaa kulikoo SHILLING 500?kha!!!!!!!!!!!!

Mimi ni msichana mwenye miaka 24 nina mpenzi wangu wa miaka 2 sasa anaonekana ni mtu mwenye msimamo na ashaweka nia ya kunioa mara nyingi tu,lakini tatizo lake kubwa ni mbahili jamani,mkitoka kwenda sehemu kula basi cost lazima mtashare hata kama ni cheap tu lakini bado ataka mshee bill au anaeza kulipa lakini mbele ya safari akakuomba umnunulie kitu kama kufidishia ile,ukimuomba vocha basi akikutumia nyingi ni 500,sasa hali hii kwa kweli ilikua yanikwaza juz nikaamua kumuomba elfu 50000 tu nina shida aliniuliza maswali jamani mpaka nikakagahishwa nikamwambia aache tu,then nikakaa muda tu hivyo after sometime nikaona ngoja nimtest tena nikamtumia sms kwamba ntakua simtafuti sana cause sina hela ya kutosha kuweka kwenye simu..what happened ni kwamba alikuwa akinitafuta tu alipotaka kuongea na mimi basi lakini hata kutuma hela ya mimi personally hakuna,na isitoshe baadhi ya ndugu zake esp mdogo wake hunitumia sms za kuniomba hela au vocha,hv huyu anafaa kua nae? hata kama wanasema mapenzi sio hela hii nashindwa elewa...nilichosahau kusema hapo juu ni kwamba ana kazi yake nzuri tu inayomlipa vizuri tu...Nishaurini jamani
120 comments

Inawezeka hana uwezo?!......

Naombeni ushauri nina mchumba ambae tunapendana sana mpole,mstaarab na muelewa kabla yangu alikuwa anatembea na mzungu na wakazaa,ila baadaye mzungu akamtenda kaka wa watu vibaya ,alimshauri afanye vasectomy,mkaka akafanya,baada ya muda wakaachaa. ndio nikawa na huyu kaka na anataka tuishi wote nifanyaje na yeye hana uwezo wa kuzalisha tena au?.24 comments

Starehe hamna kabisa.......

Msaada Tutani wa dada wenzangu,nina tatizo linalo ninyima raha muda wote hata nikiwa na mwandani wangu nashindwa kuwa huru,nina tatizo la harufu ya mbaya mdomoni nimejaribu kutumia kila aina ya dawa za mswaki bado hali si shwari,nimejaribu kusutua kwa dawa za maji bdo si shwari,msaada wenu kama kuna mtu anayejua dawa nzuri naomba anisaidie.aisha
13 comments

Miaka 6 Bado hayaishi kutokaaa....

Habari dada Dee,mie ni binti wa miaka 29,na mungu amenibariki mtoto mmoja mwenye miaka 6 kwa sasa,ila nina tatizo moja ambalo linanisumbua na pia mwenza wangu ni kutokwa na maziwa hadi leo hii,kuna kipindi niliwahi kuhisi labda sababu nilichelewa kumuachicha ziwa mwanangu au nini?nahisi wapo wanaojua harufu ya maziwa jamani,sasa sijielewi kama ni tatizo au ni dawa za kuzuia mimba ndiyo zinaleta habari hii?naomba unisaidie mpendwa kuniulizia kwa wadau wako.Ahsante.Jullien ,Dodoma.
6 comments

Mission Town hizi?

Mikasa ya dunia, kuna mdada kaolewa na kuzaa. Mume ni mission town, mke mfanyabiashara. Mwanamke ndio bread winner wa ndoa maana biashara yake ina msimamo na inaleta faida sana. Jumamosi kuna kijana kamtembelea mke nyumbani, akajitambulisha na kuelezea kilichompeleka. Alichokisema ni kwamba, samahani aunty mume wako amekua anatembea na mchumba wangu kwa miezi kadhaa sasa, nimeligundua wiki hii kwa ushahidi kabisa ndio maana nimekuja kwako. Nakuonea huruma shauri unahangaika sana kutafuta maisha kwa ajili ya watoto wako. Mwambie mume wako pole, na naomba umpatie hii bahasha. Mgeni akaondoka. Mke kufungua bahasha, ndani amekuta ni matokeo ya afya ya yule kijana na mchumba wake toka angaza, na pia madawa ambayo wamekua wakitumia (ARV's) ktk kipindi chote cha mwaka. Mke akamsubiri mumewe akamkabidhi bahasha, mume akaisoma, akaiweka pembeni na kuendelea na siku yake kama hakuna kilichotokea. Ikiwa wewe ni mke unafanyaje????
12 comments

Kweli Ushoga kazi!!!!

Habari dada,naomba unisaidie hili swala,nina rafiki yangu wa kike,urafiki wetu wa miaka kama 8 sasa,ila tangu mwaka jana dec,simuelewi shoga yangu kabisa ananiletea tabia za usagaji,tunaweza kwenda diiner wote ,akishalewa tu yaani anataka kunubusu,kunishikashika maziwa,sasa nikamuuliza kwanini unapenda kufanya hv ,akanijibu anapata hisia nami,mie nikamjibu siwezi kufanya kitendo hicho naye,kwanzia hapo shoga ananichunia,nikimtafuta ananiwekea pozi.jamani mnajua maana ya urafiki nimeshamzoea shoga yangu ila vitendo vyake vyanishinda,je nitamsaidiaje aache hivyo vitendo?
11 comments

Mapenzi yamenipiga teke mie...........

Dada pole kwa kazi nzito ya kushauri, naitwa hilda miaka 24 nilijiingiza kwenye mahusiano namvulana mmoja ambaye nampenda sana tulikua tunasoma wote chuo kimoja baada ya kumaliza chuo kila mmoja akaenda kwao tuliagana vizuri,  akaniahidi kuwa baba wa wanangu baada ya muda. kila mmoja akiwa kwao mawasiliano yakawa yamepungua nikawa namlalamikia sana juu ya yeye kutokunitafuta. Dada nisikufiche huyu mvulana nampenda sana hili lilinipelekea kuwa na wivu sana juu yake nikahisi naibiwa kwa sababu tulipokua wote chuo alipenda kuniambia ananipend sana ila baada ya kuagana hakuwa ananiambia tena. Siku moja nikamuuliza kwa nini hanitamkii tena kama ananipenda hakunipa jibu la moja kwa moja nakumbuka hiyo siku nilimlalamikia sana. Siku moja akanitumia sms akaniambia amechoka kulaumiwa hataki tena uhusiano nililia nikajaribu kumplease akakataa akasema anataka tuwe marafiki tu. Kiukweli nampenda sana natamani arudishe moyo wake kwani ni yeye wa pekee katika moyo wang. Naomba nishauri nifanyeje sababu nimechanganyikiwa
12 comments
 
Copyright © 2011. Ladies Chat - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger